Waziri Makamba afanya ziara nchini Rwanda. Waziri Biruta asema uhusiano baina ya Rwanda na Tanzania ni mfungamano wa kiundugu unaozidi kustawi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. January Makamba, aliwasili nchini Rwanda Machi 11 kuanza ziara ya kikazi ya siku nne. Katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Mhe. Dr Vincent Biruta, viongozi hao na wasaidizi wao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Rwanda na Tanzania. Hii ikihusisha masuala kama vile miradi ya uwekezaji iliyopo hadi sasa, biashara, nishati na miundombinu.

Waziri Biruta alisema ni nia ya dhati kwa Rwanda kuendelea kuimarisha mahusiano yake ya kiujirani na Tanzania, kupitia kuongeza kasi ya biashara na kuvuna kwa pamoja matunda ya ushirikiano wa kiuchumi. “Mbali ya kuchochea ukuaji wa uchumi, ushirikiano huu wa kibiashara vile vile unaimarisha mfungamano wa kiundugu baina ya hizi nchi mbili”, alisema Dr Biruta kwenye mkutano wa pamoja na wana habari.
Mbali ya kukutana na viongozi kadhaa katika Serikali ya Rwanda na kujadili mikakati ya kuimarisha uhusiano, Waziri Makamba katika ziara yake nchini Rwanda, alikutana na wanafunzi zaidi ya 100 kutoka vyuo vyuo vikuu na kufanya nao mazungumzo ndani ya African Leadership University (ALU). Mazungumzo hayo yalitazama masuala mbalimbali ikiwemo muungano wa kiuchumi wa Afrika ya Mashariki, utamaduni, michezo na muunganiko wa watu.

Waziri Makamba na ujumbe wake waliweza pia kumtembelea Mhe. Rais Paul Kagame wa Jamhuri ya Rwanda na kuwasilisha salamu kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Makamba katika habari yake aliyotupia katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika kwa kirefu masuala mbalimbali yaliyojiri katika ziara yake nchini Rwanda. https://twitter.com/JMakamba/status/1767968474427482376
Anahitimisha kwa kuandika “Mahusiano baina ya nchi zetu hizi mbili daima yamekuwa imara sana.Yanaendelea kusonga mbele katika viwango vya juu. Kama wana diplomasia, tunaishi ili kuimarisha mahusiano”.
Rwanda inajizatiti kama moja ya wazalishaji wakuu wa tungsten duniani, ikiwa ya 7 duniani na ya kwanza barani Afrika. Mafanikio haya yanatokana na Mgo…
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Rwanda…
Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiagana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Fatou Harerimana mara baada ya…
On 13th May, 2024, Rwanda High Commission in Tanzania administered an oath, and issued a Certificate of Rwandan Nationality, to Ms. Anoek De Smet, a…