| News |

Balozi Fatou akutana na wanachama wa RCA, asisitiza kupendana na kushikamana

Jioni ya tarehe 28, Oktoba 2023, Mheshimiwa Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Fatou Harerimana, aliwakaribisha wanachama wa Jumuiya ya Wanyarwanda waishio jijini Dar es salaam (RCA-Dar es Salaam) katika bustani iliyopo katika ubalozi, na kujumuika pamoja na kufahamiana zaidi.

Ilikuwa ni jioni nzuri iliyopambwa na fursa murua ya kuzungumza kwa pamoja juu ya mambo mbalimbali yanayowahusu kama jumuiya, familia, na taifa la Rwanda, kwa dhamira ya kuimarisha umoja, mshikamano, kusonga mbele na kutengeneza simulizi mpya za mafanikio (UBUMWE N'UBUDAHERANWA)

Mheshimiwa Balozi aliwasihi jumuiya kuzidi kupendana siku zote. Alisema katika hali yoyote ile migawanyiko isipewe nafasi, bali kushirikiana katika raha na shida, na kufunguliana milango ya mafaniko katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Wakati huo huo, Mhe. Balozi Fatou, aliwakumbusha wana jumuiya kuzidi kuwalea watoto wao katika maaadili ya Kinyarwanda. Alisema inahitajika umakini mkubwa wa kuwalinda watoto na kuwalea vyema katika nyakati hizi za utandawazi na maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano.

Whatsapp

  | Economic |

Rwanda yakomaa na uzalishaji wa Tungsten

Rwanda inajizatiti kama moja ya wazalishaji wakuu wa tungsten duniani, ikiwa ya 7 duniani na ya kwanza barani Afrika. Mafanikio haya yanatokana na Mgo…

Read more →
  | Diplomacy |

RWANDA REJECTS SADC SUMMIT ACCUSATIONS AGAINST THE RDF

Rwanda rejects the accusations against the Rwanda Defence Force (RDF) made in the statement of the Extraordinary Summit of the Southern African…
Read more →
  | Tanzania Embassy |

Balozi Mteule Nyamvumba awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Rwanda…

Read more →
  | News |

Balozi Mteule Jenerali Nyamvumba akutana na Waziri Kombo

Balozi Mteule wa Jamhuri ya Rwanda katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Gen. Patrick Nyamvumba awasilisha Nakala ya Hati za Utambulisho kwa…
Read more →
  | News |

Balozi Harerimana amaliza muda wake wa kazi nchini Tanzania, amuaga Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiagana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Fatou Harerimana mara baada ya…

Read more →
  | News |

Rwandan Community welcomes a new member

On 13th May, 2024, Rwanda High Commission in Tanzania administered an oath, and issued a Certificate of Rwandan Nationality, to Ms. Anoek De Smet, a…

Read more →
-->